Balaza la Madiwani la Manispaa ya Iringa limemchagua Mheshimiwa Daddy Johanes Igogo Diwani wa kata ya Gangilonga kuwa Naibu Meya mpya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kura 15 kati ya 26.
Uchaguzi huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Iringa tarehe 10.08.2017 siku ya Alhamisi na umeudhuriwa na wajumbe 26 walio piga kura, ambapo mgombea huyo ameshinda kwa kupata kura 15 za ndio huku kura 11 kati ya 26 zikiwa ni hapana.
Aidha Mh.Naibu Meya huyo ameshukuru wajumbe wote walioudhulia katika Uchaguzi huo kwa kumuamini na kumchagua kuwa Naibu Meya. Pia ameomba ushirikiano kwa wajumbe na Viongozi wa juu kwa siku zijazo.
Mbali na hayo Baraza hilo limefanya uteuzi mpya wa Wenyeviti wa kamati tano za kudumu za Manispaa ikiwemo kamati ya Fedha na Uongozi ambayo itaongozwa Mhe.Alex Kimbe,Kamati ya Mipangomiji na Mazingira itaongozwa na Mhe Tandessy G.Sanga,Kamati ya Uchumi,Afya na Elimu ambayo itaongozwa na Mhe. Raphael L. Ngullo, Kamati ya kudhibiti Ukimwi itakayoongozwa na Mhe.Daddy Johanes Igogo na Kamati ya Maadili itaongozwa na Mhe.Severin J. Mtitu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa