"Serikali yetu kupitia Mh. Rais Magufuli inawajali sana makundi ya Vijana, Wanawake na hata kundi la watu wenye mahitaji maalumu, ndio maana imekuwa ikitoa asilimia 10% kutoka mapato ya kila Halmashauri na Manispaa ukiwa ni mkopo utakao wasaidia kujikwamua kimaisha"
Kauli hiyo imezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mh. Ally Hapi katika hafla ya kukabidhi mkopo wa ujasiriamali kwa kundi la Umoja wa Madereva bodaboda pamoja na Umoja wa machinga Manispaa ya Iringa
Aidha tukio hilo limefanyika tarehe 17.09.2020 katika ukumbi wa Wallfare ambapo mkopo wa pikipiki 10 umekabidhiwa kwa Umoja wa Madereva bodaboda huku mkopo wa Milioni 12 ukitolewa kwa kundi la Umoja wa Machinga ambapo kwa ujumla vinagharimu kiasi cha shilingi Milioni 40,7000,000.
"Tunamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa kwa kutukumbuka vijana kama sisi na kutupatia mkopo utakao tusaidia kufanya ujasiriamali ili kujikimu kimaisha. Alisema Saidi Mathew, mmoja wa wanufaika na mkopo huo.
Nae Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa ya Iringa Bi. Mwantumu Dosi aliwataka wanufaika hao kutumia vyema mkopo huo na kujihakikishia wanajiletea maendeleo yao binafsi na sio kufanya shughuli zisizo na msingi.
Mh. Hapi aliwapongeza na kuwashukuru sana uongozi wa Manispaa ya Iringa kwa kutimiza agizo la utoaji mkopo wa wajasiriamali huku akiwataka kuendelea kuwasaidia wajasiriamali kila panapo hitajika.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa