Diwani wa kata ya mshindo Mheshimiwa Ibrahim Ngwada amechangia jumla shilingi million 44 kwa ajili ya uboreshaji wa ujenzi wa vyoo vya kisasa, na kuchangia baadhi ya vifaa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha elimu kwa wanafunzi wa shule ya msingi azimio.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kata hiyo diwani huyo amesema lengo lake ni kuboresha sekta zote katika kata hiyo bila kusahau sekta ya elimu, ustawi wa jamii michezo na uchumi.
Katika kuwasilisha ufadhili wake diwani huyo ametoa sukari kilo 50, unga kilo300, chaki box 1, pakti 2 za pipi ,taulo za kike box 2, peni 600, penseli boksi 2, daftali 1000, kompasi boksi1 ,cement na pia kuleta wafadhili kudhamini katika ujenzi huo wa vyoo vya kisasa .
Katika kuboresha sekta ya michezo mheshimiwa Ngwada amechangia michango kwenye timu mbili za mpira wa miguu ambazo ni timu ya Mtwaa na timu ya mshindo. Timu ya Mtwaa wamepata mipira mitatu kwa ajilli ya mazoezi na timu ya Mshindo waliwapewa mipira mitano na laki mbili ishirini na saba mia nane kwa ajili ya kukamilisha usajili wa timu hiyo kwa ligi ya mkoa .
Aidha ametoa wito kwa Wananchi kuendelea kujiunga na vikundi vidogo vidogo vya kuwainua kiuchumi ili waeweze kufaidika na mkopo mbalimbali inayotolewa na Manispaa ya Iringa
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa