KATA YA GANGILONGA YAENDELEA KUWAKINARA WA USAFI MANISPAA YA IRINGA
Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mh. Alex Kimbe ameipongeza kata ya Gangilonga kwa kuendelea kuwa kinara wa usafi wa mazingira kwa mwaka 2016/2017.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa Baraza la wazi la madiwani lililofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa tarehe 3/08/201
Kimbe amezitaka kata zingine kuiga mfano wa kata ya Gangilonga kwa kuhakisha wanasimamia usafi wa mazingira iliwaepukane na tatizo la magonjwa yamlipuko kama kipindupindu.
Aidha amesema kuwa wakati ujao Manispaa imejipanga kutoa zawadi ya pikikipi ya miguu mitatu kwa mshindi wa kwanza hivyo kama kata wanatakiwa kujitaidi iliwaigie kwenye hicho kinyang’anyilo.
Kata zingine zilizo jitaidi kwa usafi kwa mwaka huu ni pamoja na kata Mlandege kwa nafasi ya pili ikifutatiwa na Kitanzini kwa nafasi ya tatu huku kata ya Igumbilo ikivunja rekodi kwa kushika nafasi ya mwisho.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa