Iringa Manispaa ni miongoni mwa Wilaya 65 Tanzania zinazotekeleza mradi wa HEBU TUYAJENGE chini ya ufadhili wa Shirika la Misaada la watu wa Marekani( USAID) chini ya usimamizi wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na maambukizi ya VVU UKIMWI
Shirika la Centre for women and children development(CWCD limeendesha mafunzo hayo kwa timu ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhusu gurudumu la rufaa(Bi-directional referrals and linkeges) kwa lengo la kuongeza uelewa kwa waheshimiwa Madiwani kutoka kata 5 za mradi ambazo ni Kihesa,Mkwawa,Igumbilo, Isakalilo na Ruaha. Katika kutekeleza mradi huo Madiwani pamoja na wataalam wamepewa mafunzo ya namna ya kuibua vijana na watoto wenye viashiria vya VVU UKIMWI ili waweze kupimwa afya zao na kuanza kutumia dawa
Akitoa mada katika mafunzo hayo Bi.Happy Josephat amesema iko tamko la Serikali kuhusu ridhaa ya vijana wenye umri wa miaka 15 linaelekeza kuwa kijana mwenyewe anayo ridhaa ya kupima VVU UKIMWI bila ridhaa ya mzazi hivyo amewataka wajumbe kutoa elimu hiyo katika jamii
Ameeleza kuwa changamoto kubwa kwa vijana kutojitokeza kupima VVU UKIMWI ni ukosefu wa huduma rafiki kwa vijana kwenye vituo vya afya hivyo kupelekea vijana kushindwa kujitokeza kupata huduma
Aidha amesema malengo ya kimkakati ni kuhakikisha wanafikia asilimia95 watu kupima VVU UKIMWI 95 waliopima wenye maambukizi waanze dawa 95 Wabaki kwenye dawa ili kufubaza VVU kwenye damu
Bi.Josephat amesema mpango kazi waliojiwekea kwenye mafunzo hayo ni Halmashauri kuhakikisha inaibua vijana na watoto,pia wenye maambukizi ya VVU kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika vikao vyote vya Kata na Mitaa ili waweze kutoa elimu
Kwa upande wake Naibu Meya mhe.Kenyata likotiko amelishukuru Shirika la CWCD kwa kutoa mafunzo hayo kwanikwa watu sahihi na kuwa wao ndiyo viongozi wa wananchi itakuwa rahisi kuwafikishia elimu waliyoipata na kuleta matokeo tarajiwa
Mheshimiwa Eliud Mvela ni Mwenyekiti wa huduma za jamii anasema kazi kubwa waliyonayo ni kufanya kazi kwa ushirikiano kati ya Madiwani wataalam,viongozi wa Konga ili kuifikia jamii kwakufanya ufatiliaji wa karibu ili kutimiza mpango mkakati waliojiwekea
Kaimu Mkurugenzi Dr.Jesca Lebba amesema atahakikisha mikakati yote iliyowekwa inatekelezwa kwa wakati na kuahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi wa konga pindi watakapopata changamoto za kitaalam wakati wanatekeleza majukumu yao
Mafunzo hayo yamefadhiliwa na USAID,PEPFAR,CWCD na NACOPHA yamefungwa leo tarehe 10/7/2021 na Katibu Tawala Wilaya ndugu Eston Kyando ambaye amewataka washiriki kuyatendea kazi ili yaweze kuleta matokeo chanya.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa