Wakuu wa Idara pamoja na Vitengo wa Manispaa ya Iringa wamepata elimu juu ya mafunzo ya mfumo wa kieletroniki wa uandaaji wa Bajeti mbalimbali.
Mafunzo hayo yamefunguliwa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bw. Omary Mkangama katika ukumbi wa Lugalo Sekondari, ambapo amewataka washiriki kuzingatia mafunzo hayo ili muda wa kuandaa bajeti unapofika basi Manispaa ya Iringa isipatikane kasoro yoyote katika matumizi ya mfumo na kuweza kuwasilisha mabeti sahii kwa manufaa ya maendeleo ya manispaa nzima ya Iringa.
Aidha, akizungumza Mratibu wa mafunzo hayo Musifwaki Haule amesema madhumuni makuu ya Mafunzo ya mfumo wa kieletroniki wa uandaaji wa Bajeti (Planrep Training) ni kupata elimu ambayo itawasaidia wakuu wa Idara na Vitengo katika kuandaa bajeti ya matumizi ya Manispaa ya Iringa.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuhitimiswa siku ya alhamisi tarehe 28/9/2017.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa