Mkuu wa Wilaya ya Iringa,Mheshimiwa Richard Kasesela ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Iringa kwa kushirikiana na Afisa Tarafa wa Manispaa ya Iringa, kuchukua sensa ya wananchi wote waliovamia na kujenga milimani ili kuweza kuwapatia namba za utambulisho na kudhibiti kutokutokea kwa uvamizi mwingine zaidi ya wale waliotambuliwa na kupewa namba.
Mkuu huyo wa Wilaya ameahidi kufanya mkutano katika eneo hilo na kuahidi kuunda kikosi kazi cha ulinzi katika eneo hilo ambacho kitasimamia kuangalia wananchi waliopo katika eneo hilo na kufanya wananchi wengine kutokuvamia milima hiyo. Mkutano huo wa hadhara wa mkuu wa Wilaya na wananchi waliojenga milimani utafanyika baada ya sense ya kujua nyumba zilizo milimani kukamilika.
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ametembelea eneo la makaburi la igeleke na kuwataka wale wote walovamia eneo hilo kupigwa faini na kutakiwa kutoka katika eneo hilo.
Milima na vilima vinatakiwa kutunzwa ili kutunza mazingira kwani kwa kukata miti na kujenga milimani husababisha ukame na zaidi hufanya miundombinu ya maji safi na maji taka kushindwa kuwapo hivyo kupelekea kusababisha magonjwa ya mlipuko na magonjwa ya tumbo kwa wananchi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa