Timu ya watumishi kutoka Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za mitaa imeishauri Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha wanaongeza ufanisi katika Miradi ya Maendeleo na kuwashirikisha wananchi katika shughuli zote zinazofanywa na manispaa hiyo ili kuipunguzia Serikali mzigo wa gharama za ujenzi wa miradi hiyo.
Ushauri huo umetolewa wakati wa Ziara ya kamati hiyo ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 ili kujua hali ya miradi hiyo.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na Ujenzi wa soko la Ngome, Ofisi ya mtendaji wa kata ya Mtwivila, Ujenzi wa Shule ya msingi Mawelewele na Ujenzi wa Barabara ya Don Bosco - Mawelewele.
Licha ya timu hii ya watumishi kutoka Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na Serikali za mitaa kutaka kujua hali ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pia ilikuwa na lengo la kufahamu Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa kupitia mfuko wa jimbo, makusanyo ya Mapato ya ndani, utengaji wa maeneo ya Biashara, Viwanda na uwekezaji pamoja na kujua Maendeleo ya utoaji wa Elimu msingi bila malipo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa