Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Joseph Lyata amewataka wajumbe wa kamati ya Mipango na Mazingira kuhakikisha wanaifanya Manispaa kuwa ya kijani kwa kusimamia usafi wa Mazingira na kuhamasisha Wananchi kupanda miti ili kuwa ya mfano kwa manispaa nyingine hapa nchini.
Lyata ameyasema hayo wakati wa mafunzo ya usafi wa Mazingira kwa wajumbe wa kamati ya Mazingira na Mipango Miji yaliyofanyika katika ukumbi wa Community Center tarehe 5/07/2017 mpaka tarehe 06/07/2017.
Mada zilizofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na maana ya Mazingira na vitu vilivyomo ndani yake, sheria zinazosimamia Mipango Miji na Mazingira, na faida za utunzaji wa Mazingira.
Mafunzo haya ya Mipango na Usafi wa Mazingira kwa wajumbe wa kamati yaliandaliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa lengo la kuwajengea uwezo wajumbe hao juu upangaji wa Mji na Usafi wa Mazingira, wajumbe hao wa kamati ni kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka ngazi ya mitaa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa