• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

MGANGA MKUU WA MANISPAA YA IRINGA AMEWATAKA WANAWAKE VINARA WA LISHE KUTOA ELIMU YA MLO KAMI

Posted on: August 13th, 2020

Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Dr.Jesca Lebba amewataka wanawake vinara wa lishe kuhakikisha wanatoa Elimu ya mlo kamili

 ili Kuketa mabadiliko katika jamii.

Dr.Lebba ameyasema hayo leo katika ukumbi wa Hall mark  kata ya Mkimbizi Manispaa ya Iringa wakati akifungua semina ya siku moja iliyowashirikisha wahudumu wa afya katika ngazi ya jamii pamoja na baadhi ya wataalamu wa lishe ngazi ya Halimashauri pamoja na ofisi ya mkuu wa Mkoa.

Dr.Lebba amesema bado wanawake vinara wanao wajibu wa kuelimisha jamii kuanzia katika ngazi ya familia kuhusu mlo kamili na kuwa wao ndio wanatakiwa wawe mfano wa kuigwa wanatakiwa kuhakikisha jamii inajenga utamaduni wa kula  makundi matano ya vyakula ili kuhakikisha wanatokomeza tatizo la udumavu na utapiamlo.

Dr.Lebba anashangazwa na takwimu za utapiamlo katika Mkoa wa Iringa kuwa ni asilimia 47 na kuwa Mkoa unaongoza kwa kushika nafasi ya pili kitaifa ilihali uzalishaji wa  mazao ya chakula  ni wa kiwango cha juu.

Akitoa mada katika mafunzo hayo Afisa lishe  Manispaa ya Iringa Bi.Anzael Msigwa amesema ni vyema kina mama wajawazito kuhakikisha wanawahi kuanza clinic mapema kabla ya miezi mitatu ili kunusuru afya ya mtoto na udumavu pamoja na magonjwa mengine.

Msigwa anasema ni vema mtoto apate vichanganshi tangu akiwa mdogo ,pamoja na mama mjamzito kula mlo kamili,na kupata huduma za awali toka kwa wataalam pindi anapowahi kuanza clinic kwani kwa kufanya hivyo Itasaidia sana mama mjamzito kujifungua mtoto mwenye afya njema .

Happiness Siliwa muwezeshaji kutoka lishe endelevu anasema mradi huu wa miaka mitano  umumefadhiliwa na USAID kwa kushirikiana na wadau wengine kama  Deloit,African Academy, na Save the Children unafanya kazi katika Mikoa minne ambayo ni Iringa,Dodoma,Morogoro na Rukwa,na umepanga kuwafikia wanawake wapatao milioni moja na laki tano,vijana pamoja na watoto.

Mafunzo hayo yenye jumla ya washiriki thelasini yamefunguliwa na kufungwa na Mgeni rasmi Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa.

Matangazo

  • MANISPAA YA IRINGA YANG'ARA MATOKEO KIDATO CHA PILI NA CHA NNE 2020. January 15, 2021
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI MANISPAA YA IRINGA 2021 March 05, 2021
  • TANGAZO LA KAZI : MANISPAA YA IRINGA 23.09.2020 September 23, 2020
  • IMC: ORODHA YA MAJINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MKUU 2020 PAMOJA NA MAENEO YAO YA KUFANYIA SEMINA. October 24, 2020
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • PUMZIKA KWA AMANI HAYATI DR. JOHN MAGUFULI : DAIMA TUTAKUKUMBUKA

    March 25, 2021
  • MADIWANI MANISPAA YA IRINGA WAGAWA ZAWADI ZILIZOTOLEWA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

    March 13, 2021
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MANISPAA YA IRINGA YAFANA. WANAWAKE WAJITOKEZA KWA WINGI

    March 08, 2021
  • WANAWAKE MKOANI IRINGA WAJIPANGA KULETA MABADILIKO CHANYA KUELEKEA KILELE MAADHIMISHO YA MWANAMKE DUNIANI

    March 04, 2021
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa