Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Iringa Mjini ndugu Said Lubeya ameupongeza Uongozi wa Manispaaa kwa kufanya vizuri katika ujenzi wa Miradi ya vyumba vya Madarasa ya Shule za Sekondari zilizopo Manispaa ya Iringa
Lubeya ameyasema hayo leo tarehe 26/01/2021 katika ziara iliyohusisha Miradi hiyo na kuona jitihada zinazofanywa na timu ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha wanafunzi 907 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2021 wanapata nafasi hiyo bila usumbufu wiwote
"Nikuombe Mkurugenzi usimamie vizuri zaidi kuhakikisha Walimu na wanafunzi wanapata vyoo imara kwa uwiano wa kitaalamu kwa walimu na wanafunzi" alisema Lubeya
Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Hamid Njovu amewapongeza Kamati ya Siasa Wilaya kwa kuwa bega kwa bega kuiletea maendeleo Halmashauri ya Manispaa
Akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahimu Ngwada amesema anampongeza sana MNEC Salim Abri kwa moyo wa kujitolea kila wakati kusaidia ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo madarasa na ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Mstahiki Meya na Mbunge Mhe. Jesca Msambatavangu
Ngwada amesema Halmashauri iko tayari kupokea maelekezo na maagizo na kuyafanyia kazi kwani wamedhamiria kufanya mabadiliko makubwa katika Baraza hili jipya la Madiwani liloanza kazi muda mfupi uliopita
Miradi iliyotembelewa leo na kamati ya Siasa ya Wilaya ni pamoja na Shule ya Sekondari ya Nduli, Zahanati ya Nduli, Shule ya Skondari Umoja, Mkwawa, Mlamke, Ipogolo na Igumbilo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa