"Lengo letu ni kuhakikisha tunafuata sheria, kanuni na taratibu katika kuendesha vituo vya kulea watoto mchana (Day Care) na shule za awali ili tusivunje sheria na baadae kupelekea kuwayumbisha watoto wasio kuwa na hatia yoyote" Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu alipokuwa alkizungumza na wamiliki wa Shule za awali na shule za watoto za mchana katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Waratibu wa Elimu kata, Maafisa Ustawi wa Jamii ngazi ya Mkoa na Wilaya pamoja na Afisa Elimu Taaluma ngazi ya Mkoa Ndugu Edina Byemerwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa