Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Ally Hapi ametoa siku 14 za kukamilishwa kwa majengo ya madarasa pamoja na ukarabati wa madawati ya wanafunzi kwenye shule zote zenye changamoto hizo zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Maagizo hayo ameyatoa katika ziara yake ya terehe 19.01.2021 wakati akitembelea na kukagua miradi ya ujenzi wa baadhi ya madarasa ya shule za Msingi na Sekondari ndani ya Manispaa ya Iringa akiwa ameongozana na wataalamu mbalimbali kutoka Mkoani na Halmashauri.
Aidha Mh. Hapi amekemea tabia ya baadhi ya viongozi wa shule kushindwa kusimamia sheria na taratibu za Sekta ya Elimu kwa walimu wengi kutofundisha kwa weledi muda wa vipindi na badala yake wanafundisha muda wa ziada wa jioni ili waweze kujipatia malipo(posho)
Hapi amesema, tatizo hilo linapelekea wanafunzi wengi kuchelewa kurudi majumbani hali ambayo ina hatarisha usalama wao hasa wanafunzi wa kike
Hata hivyo Mhe. Hapi ameipongeza Manispaa kupitia Mstahiki Meya Mhe. Ibrahim Ngwada kwa jitihada anazozifanya za kupunguza changamoto ya upungufu wa madawati ya wanafunzi ambapo kupitia Mstahiki Meya huyo ameweza kutafuta wadau mbalimbali wa elimu kuchangia zoezi hilo
“Watoto wote waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka 2021 na wanaostahili kuwa shuleni basi wapelekwe mashuleni, Jeshi la polisi litashughulika na wazazi ambao ni wazito kuwapeleka watoto hao” kauli ya Mkuu wa Mkoa huyo mara baada ya kutambua kuwa kuna wanafunzi wengi bado hawajafika mashuleni kwenye usali wa kuanza masomo yao.
Sambamba na hilo Mh. Hapi ameipongeza Manispaa ya Iringa kwa kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha Pili na cha Nne kwa mwaka 2020 na kuwataka walimu walimu waongeze Juhudi kufikia nafasi ya kwanza kitaifa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa