Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza ameendesha kikoa na viongozi wa Dini chenye lengo la kubaini changamoto za kijamii hususan ukosekanaji wa maadili kwa watoto na ukatili wa kijinsia.
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa siku ya jumatatu ya Tarehe 20/11/2017 ambapo wazee mbalimbali waliweza kutoa maoni yao ilikuwea kutokomeza tatizo hilo.
Masenza amewataka viongozi wa Dini kupambana dhidi ukatili wa jinsia na pia kushirikiana kikamilifu kubainisha na kuanzisha vikundi vya kutoa elimu kuhusu suala la malezi kwa watoto ili kuepuka ukatili huo na Magonjwa mengine kama Ukimwi, na magonjwa ya mama na mtoto wakati wa kujifungua huku akisisitiza kupima afya mara kwa mara ili kuweza kujua afya zao.
Aidha Masenza ametoa ufafanuzi juu ya usajili unaowahusu Waganga wa Jadi ambao viongozi wadini wameitupia lawama serikali kwa kuwapa vibali vya usajili jambo ambalo linaongeza vitendo vya kikatili Mtaani nakusema kuwa serikali aiungi mkono swala hilo na pia wanasajili waganga wa tiba za asili na sio wanaopiga lamri.kama inavozaniwa.
Naye askofu mstafu wa kanisa la KKKT jimbo la Iringa ameshauri kuwa linatakiwa litegenezwe jukwaa na kamati ya viongozi wa dini watakao kuwa wanazungumzia matatizo ya maadili ilikuweza kutengeneza jamii mpya ya watu wa Iringa wenye maadili mema.
Mada mbalimbali zilitolewa kutoka kwa wataalum wa Ofisi ya Katibu Tawala wa mkoa ambazo zilikuwa zinaeleza hali ya maadili kwa mkoa wa iringa ikiwemo ukatili wa kijinsia.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa