MKUU WA MKOA WA IRINGA AMEZINDUA RASMI SHINDANO LA MAMA MSOSI LISHE.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza amewataka wananchi wa Manispaa ya Iringa kuzingatia lishe Bora ili kuepuka maradhi yanayotokana na ukosefu wa virutubisho ambayo ni Udumavu,Vichwa vikubwa, Utapiamlo, pamoja na mgongo wazi.
Masenza ametoa wito huo katika uzinduzi wa shindano la Mama Msosi Lishe ambalo limefanyika katika Bustani ya Manispaa ya Iringa (Garden) siku ya jumamosi Tarehe 11/11/2017 lenye lengo la kuhamasisha lishebora kwa familia,usafi wa mazingira, pamoja na matumizi ya nishati mbadala.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Dr.Isesande Kaniki,amwa uhakikishia umma kuwa zoezi hilo litazingatia vigezo vyote vilivyowekwa kwani uongozi umejipanga vizuri kwa kuanzia ngazi ya chini mpaka juu kwani kuna wataalamu wakutosha kusimamia shindano hilo.
Kampeni hiyo imehudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi, wataalamu wa afya ,watumishi wa umma ngazi ya mkoa na manispaa,wadau waafya na lishe,vikundi vya wajasiriamali,wahudumu wa afya ya jamii na wananchi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa