Mkuu wa mkoa wa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi amekabidhi kompyuta (20) kwa shule za sekondari mkoani Iringa zilizotolewa na mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) chini ya msaada wa Mbunge wa viti maalum Iringa Mjini Mheshimiwa Ritha Kabati.
Akizungumza wakati wa kukabidhi kompyuta hizo mkuu wa Mkoa Mh. Hapi ameushukuru mfuko wa mawasiliano kwa wote na kwa kushirikiana naMheshimiwa Mbunge wa viti maalum Ritha Kabati kwa udhamini wao na kuweza kufanikisha kupatikana kwa kompyuta hizo na kutoa wito kwa waalimu zitumike kwa umakini kwani zitasaidia sana wanafunzi katika kujifunza na kuongeza ubunifu kwa wanafunzi mkoani Iringa.
Aidha akitoa shukrani zake Mbunge Ritha Kabati amesema ameamua kusaidia shule za sekondari mkoa mzima baada ya kuona changamoto ya kompyuta katika baadhi ya shule ambapo ametoa Jumla ya kompyuta 20 . kompyuta 11 zitaenda katika shule zilizopo katika Manispaa na nyingine zitapelekwa katika wilaya za mkoa wa Iringa.
Viongozi mbalimbali wa serikali walihudhuria kwenye makabidhiano hayo akiwemo Naibu Meya Manispaa ya Iringa Mheshimiwa Nzala Ryata, Mkurugenzi Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu, Kaimu mkuu wa wilaya na viongozi mbalimbali wa Chama Cha mapinduzi ngazi ya mkoa na wilaya
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa