Afisa wa Takukuru Aneth Mwakatobe ametoa elimu kuhusiana na mapambano dhidi ya rushwa kwa watendaji wa Kata pamoja na watendaji wa Mitaa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Ukumbi wa Community Center.
Elimu hiyo ya kupambana na rushwa katika maeneo ya kazi, imetolewa baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi kuhusiana na utendaji dhaifu wa kazi kwa baadhi ya watendaji wa kata
Aidha Mwakatobe ametoa ufafanuzi kuwa moja ya kazi za Takukuru ni kutoa Elimi dhidi ya Rushwa, kufanya Uchunguzi wa malalamiko yanayotolewa kisha kumkamata mtuhumiwa na kumpeleka Mahakamani endapo watabaaini amejihusisha na kitendo cha rushwa.
Aidha watendaji wa Mitaa na Kata wametoa maoni na changamoto kwa TAKUKURU ambapo wameahidi kuzifanyia kazi huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa kuzingatia Maadili na Haki kwa kila mmoja kama Mlengo wa Serikali ya awamu ya tano inavyowataka dhidi ya kupambana na Rushwa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa