‘’Niwapongeze Wananchi wote wa Kata ya Isakalilo kwa kujitokeza kwa wingi na pia idara ya Mipango Miji kwa kuendeleza kampeni ya kupanda Miti katika mipaka ya Manispaa yetu ya Iringa “
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela katika uzinduzi wa kampeni ya upandaji Miti Kiwilaya iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Isakalilo tarehe 31/1/2020 Manispaa ya Iringa ambapo Miti elfu Moja imepandwa.
Aidha amewaomba Wananchi kulinda Miti waliopanda na kuwaomba kutoa taarifa kwa wale wote wanaobeba Mkaa kwa kutumia pikipiki bila kibali.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa