Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi Amina Masenza amewataka Wananchi wote wa Manispaa ya Iringa kuwa na utaratibu wa kufanaya mazoezi ili kuepuka mangonjwa yasioambukizwa
Bi Masenza ametoa wito huo katika zoezi la upimaji wa Afya bure ambalo limeziduliwa katika uwanja wa Samora na kuhamia katika Bustani ya Manispaa ya Iringa (GARDEN) siku ya jumamosi Tarehe 18/11/2017 ambapo magonjwa mablimbali yamepimwa bure ikiwemo Kisukari,Presha,Uzito,Uchunguzi wa Saratani ya matiti na mlango wa kizazi,Upimaji wa virusi vya Ukimwa, pamoja na Uchangiaji wa Damu kwa Hiari.
Mbali na hayo amewataka viongozi wa Taasisi mbali mbali za kidini na za Umma kutoa elimu kwa Wananchi juu ya umuhimu wa kufanya mazoezi na kuwa na Ratiba ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujua hadhi ya afya zao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa