WANUFAIKA NA MPANGO WA TASAF-III WAPONGEZWA KWA MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA ZA TASAF
Wanufaika 153 wa mpango wa TASAF-III katika Manispaa ya Iringa hususan Kata ya Mkwawa, Kitwiru na Kata ya Ruaha wamepongezwa kwa matumizi sahihi ya fedha za mpango huo ambazo zinatolewa kwa lengo la kusaidia kaya zilizokatika mazingira hatarishi kujinasua katika umaskini.
Akizungumza na wanufaika wa kata ya Mkwawa, Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Joseph Chitinka amesema kuwa inatia moyo kuona fedha zinazotolewa na mpango zinafanya shughuli kusudia za maendeleo ikiwemo ufugaji, elimu, ujasiliamali na kuanzisha vikundi vya hisa.
Amesema kikundi cha Hisa kilichoanzishwa na wanufaika wa Kikundi cha Lukosi kilicho katika kata ya Mkwawa kimeweza kuzalisha mtaji hadi kufikia shilingi laki saba, ambapo kila baada ya kupewa fedha kutoka TASAF kila mnufaika anachangia shilingi 5000/- katika kikundi hicho na baadae wanachama wanakopeshana na kuzalisha faida hivyo kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo na kuhudumia jamii na familia zao.
Aidha, Katibu Tawala huyo ametoa agizo kwa watendaji wa Kata ya Mkwawa kuhakikisha wanufaika waliotoa fedha na kupigwa picha kwaajili ya kupata vitambulisho vya tiba kwa kadi (TIKA) wahakikishe baada ya miezi mitatu wanufaika hao wamepewa kadi hizo za matibabu.
Manispaa ya Iringa ina jumla ya Mitaa 98 ambayo inanufaika na mpango huo wa TASAF wa kunusuru kaya masikini kati ya mitaa 192 na ina jumla ya walengwa 2925 kwa kata 18 za Manispaa ya Iringa.
You are wanufaika with the tasaf plan-III.
Wanufaika 15
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa