• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

WATENDAJI WATAKIWA KUHAKIKISHA WANATIMIZA MAJUKUMU YAO KWA KUKUSANYA KODI MBALIMBALI ZA HALMASHAURI KWA WAKATI

Posted on: February 11th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Iringa ndugu Richard Kasesela amewataka watendaji kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha kodi mbalimbali zinatolewa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni zilizowekwa ili kufikia malengo ya ukusanyaji waliyojiwekea

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 11/2/2021 kwenye kikao cha kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Iringa kwa lengo la kupitia bajeti ya mwaka 2021/2022

Aidha Kasesela amesema watendajii wanajukumu kubwa kuhakikisha kodi mbalimbali zinakusanywa kwa wakati na bila bugudha na ameainisha kodi zilizorudishwa kukusanywa na Halmashauri ni pamoja na Kodi ya majengo,kodi ya mabango ambazo awali zilikuwa zikikusanywa na mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)pamoja na kuhakikisha wafanyabiashara wote wanakuwa na vitambulisho vya wajasiriamali awamu ya tatu ambavyo vitaanza kuuzwa hivi karibuni

Kasesela amesisitiza katika bajeti ya 2021/2022 ipo haja ya kuangalia changamoto ya usafiri kwa watendaji na kuhakikisha suala hilo linaingia kwenye bajeti ili kurahisisha utendaji kazi wao na kuwafanya wafanye kazi kwa weledi

Kuhusu Sekta ya  elimu Kasesela amewapongeza walimu kwa kufanya kazi kwa bidii hivyo kuufanya Mkoa wa Iringa  kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya kidato cha pili na kidato cha nne

Ameshauri bajeti ijayo katika Idara ya Elimu Sekondari izingatie suala la kambi za wanafunzi wa kidato cha nne  angalau waweze kukaa  kwa kipindi kisichopungua miezi miwili ili kuongeza ufaulu kwa mwaka 2021 katika Mkoa wa Iringa

Said Lubeya ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya amesema anawapongeza watumishi wote wa Halmashauri kwa kukusanya mapato zaidi ya lengo ililojiwekea na kusema pamoja na upungufu wa wafanyakazi uliopo bado Halmashauri imefanya vizuri katika Usafi wa mazingira,Mitihani,ukusanyaji wa mapato na shughuli zingine za kiuchumi hivyo kuwaletea maendeleo wananchi wake

Lubeya ameahidi kushirikiana na watendaji katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Madiwani wakiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa  mhe. Ibrahimu Ngwada kuhakikisha wanaonyesha tofauti ya utawala wa  CCM na CHADEMA

Mstahiki Meya Manispaa mhe.Ibrahim Ngwada amemshukuru Mjumbe wa Halmashauri kuu CCM Taifa (MNEC) Salim Abri  Asas kwa kufanya marekebisho ya jengo la ofisi yake na kusema kuna haja ya viongozi wote wa chama na Serikali kutambua kazi kubwa inayofanywa na MNEC katika jamii na kumpongeza kwa moyo wa kujitoa kwa ajili ya wananchi

Omary Mkangama ni kaimu Mkurugenzi ameahidi kuyapokea marekebisho yote yaliyofanywa katika mapitio ya bajeti hiyo na kuahidi kuyafanyia kazi mapema iwezekanavyo

Kikao cha kamati ya Ushauri ya  Wilaya hufanyika mara moja kwa mwaka na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, vyama na Serikali,Taasisi za kiraia pamoja na wakuu wa Idara na vitengo na watendaji wa Kata.

Matangazo

  • MANISPAA YA IRINGA YANG'ARA MATOKEO KIDATO CHA PILI NA CHA NNE 2020. January 15, 2021
  • TANGAZO LA KAZI : MANISPAA YA IRINGA 23.09.2020 September 23, 2020
  • IMC: ORODHA YA MAJINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI MKUU 2020 PAMOJA NA MAENEO YAO YA KUFANYIA SEMINA. October 24, 2020
  • HERI YA MTIHANI MWEMA KWA KIDATO CHA NNE 2020. November 23, 2020
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • NAIBU WAZIRI WA ARDHI MHE. ANGELINA MABULA AMEWATAKA WAKURUGENZI MKOANI IRINGA KUONGEZA NGUVU YA UKUSANYAJI WA MADUHURI YA SERIKALI

    March 26, 2021
  • MB: IRINGA MJINI ATOA SEMINA YA UJASIRIAMALI KWA MADEREVA BAJAJI

    February 24, 2021
  • MEYA MANISPAA YA IRINGA AKABIDHI KITITA CHA MILIONI MOJA TIMU YA RUAHA SPORTS ACADEMY

    February 23, 2021
  • WATU WENYE ULEMAVU WAPEWA VIUNGO VYA BANDIA MANIAPAA YA IRINGA

    February 19, 2021
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa