Halmashauri ya Manispaa ya Iringa katika mwaka wa fedha 2016/17 imepanga na kuidhinishiwa kutekeleza miradi ya Maendeleo yenye thamani ya Tsh. 13,575,883,159, kati ya fedha hizo Tsh. 11,181,579,525 ni Ruzuku kutoka Serikali Kuu na Wafadhili, na Tsh. 2,394,303,634 zinatarajiwa kuchangiwa na Halmashauri kutokana na vyanzo vyake vya mapato ya ndani. Michango ya wananchi na nguvu kazi katika kusaidia utekelezaji wa Miradi hiyo katika maeneo yao inatarajiwa kufikia jumla ya Tsh. 135,985,625.9. Bajeti hii ilizingatia maelekezo, Sera na Miongozo kama ilivyotolewa na Serikali.
Hadi kufikia Machi 2016/2017, Halmashauri ilikuwa imepokea jumla ya Tsh. 4,282,298,373 toka Serikali Kuu sawa na asilimia 38.3 ya makadirio ya fedha za Maendeleo toka Serikali kuu kwa mwaka 2016/2017. Miradi iliyopokea fedha ni pamoja na Ruzuku toka serikali kuu (LGCDG) Tsh. 190,475,000, Mfuko wa Jimbo (LCDCF) Tsh. 30,274,000, Shule Maalumu Tsh. 100,000,000, Mfuko wa Pamoja wa Afya (HSBF) Tsh. 209,109,750, Mradi wa Usambazaji maji vijijini (NRWSSP) Tsh. 29,003,449, Mradi wa Uendelezaji Mji (ULGSP) Tsh. 2,476,681,361, Mradi wa kusaidia huduma za watoto walio katika mazingira hatarishi (UNICEF) Tsh. 319,353,200 na Mfuko wa Barabara (ROAD FUND) Tsh. 927,401,613.
Mpaka kufikia Mwezi Machi 2017, jumla ya Tsh. 3,830,016,654 zilikuwa zimetumika sawa na asilimia 89.4 ya fedha zilizopokelewa.
Hata hivyo katika kipindi cha Julai hadi Machi 2016/2017 Halmashauri ilipokea jumla ya Tsh. 2,219,164,180.86 fedha za miradi nje ya bajeti ya mwaka 2016/2017, ikiwa ni fedha za Mfuko wa Barabara (Road Fund) Tsh 1,763,579,680 na Tsh. 455,584,500 ikiwa ni fedha za kusaidia kaya maskini kupitia TASAF III. Kati ya fedha zilizopokelewa jumla ya Tsh.1,852,954,500 zimetumika sawa na asilimia 83.5 ya fedha zilizopokelewa.
Mchango wa Halmashauri katika miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa kipindi cha Julai hadi Machi, 2016/2017 ni Tsh. 745,174,053 sawa na asilimia 31 ya makadirio.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa