2.0 TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA TASAF
Mradi wa TASAF kitaifa ulianza kutekelezwa kuanzia mwaka 2001-2005 kwa awamu ya kwanza, awamu ya pili mwaka 2006-2009 na awamu ya tatu imeanza kutekelezwa mwaka 2012 mpaka sasa. Taarifa za utekelezaji kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inaoneshwa katika maelezo hapa chini
2.1 TASAF AWAMU YA - I
Katika utekelezaji wa Mradi wa TASAF awamu ya I (2001-2005), Halmashauri ya Manispaa ya Iringa haikupata nafasi ya kutekeleza mradi huu. Sababu kubwa ilikuwa ni muongozo wa utekelezaji wa mradi ulielekezwa katika ngazi za Halmashauri za Wilaya tu.
2.2 TASAF AWAMU YA - II
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni mojawapo ya Halmashauri zilizopata Ufadhili kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF II) kuanzia mwaka 2006 hadi 2009. Katika kipindi hiki Halmashauri ilipokea jumla ya Tshs. 1,515,432,211 kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa madarasa 44, Maabara 1, matundu ya vyoo 116, Zahanati 2, ukarabati wa barabara 8, Vikundi 10 vya ufugaji wa kuku na nguruwe na mradi wa Mwitikio wa Jamii Dhidi ya UKIMWI (MJADU) ambao ulitekelezwa kwa mitaa 17.
2.3 MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASIKINI TASAF - III
TASAF awamu ya III ilizinduliwa rasmi na Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete mwezi Agosti, 2012 Mkoani Dodoma na utekelezaji wake ulianza kwa baadhi ya Halmashauri. Mpaka sasa Mpango huu wa Kunusuru Kaya Masikini unatekelezwa kwa Halmashauri 161 ikiwemo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini ulizinduliwa rasmi tarehe 06/01/2015 katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa. Uzinduzi huo ulijumuisha viongozi kutoka ngazi ya Mkoa, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Waheshimiwa Madiwani wa Kata zote, Afisa Tarafa, Wakuu wa Idara na Vitengo, wataalam kutoka Idara mbalimbali waliochaguliwa kuwa wawezeshaji ngazi ya Wilaya.
Katika Mpango huu wa Kunusuru Kaya Masikini jumla ya Mitaa 98 imefikiwa kati ya mitaa 192 iliyopo Manispaa ya Iringa. Jumla ya Kaya 2953 ndizo zinazohudumiwa na Mpango wa kunusuru Kaya masikini zenye jumla ya wanafunzi wa sekondari 616, wanafunzi wa shule ya msingi 2,031 na watoto wa kliniki 394 ambao hupata huduma katika shule za msingi 43, sekondari 12, zahanati 9 na vituo vya afya 4.
2.4 MADHUMUNI YA MPANGO WA TASAF - III
Madhumuni ya TASAF awamu ya III ya Mpango wa Kunusuru Kaya ni kutoa ruzuku kwa kaya za walengwa ili kuziwezesha kaya masikini kupata mahitaji ya msingi (Afya na Elimu) na fursa za kujiongezea kipato, kulinda rasilimali zao na kuweka akiba kwa ajili ya kujiletea maendeleo na hatimaye kujitoa katika umaskini
2.6 UHAULISHAJI WA FEDHA
Uhaulishaji fedha kwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ulianza mwezi Agosti, 2015. Malipo kwa kaya masikini yanatolewa kwa miezi miwili miwili. Vile vile malipo kwa kaya masikini yanategemea utimizaji wa masharti ya afya na elimu kwa kaya husika, Mpaka sasa malipo yametolewa kwa awamu kumi na moja ambazo ni mwezi Julai, 2015 – Januari, 2017 ambapo jumla ya Tshs. 1,092,868,000/=.
MAFANIKIO YALIYOANZA KUONEKANA
i) Ruzuku imesaidia walengwa kumudu kupata mahitaji ya msingi kama vile chakula kwa milo mitatu, sare na vifaa vya shule. Hii imesaidia kuongezeka kwa mahudhurio ya wanafunzi shuleni.
ii) Pia ruzuku imesaidia walengwa kujiunga na Mfuko wa Tiba kwa KAdi (TIKA) ambapo jumla ya walengwa 2464 waliunga na mfuko huo kwa mwaka 2016. Halmashauri imeendelea kuhamasisha walengwa kujiunga na TIKA mwaka huu 2017 jumla ya walengwa 936 wamejiunga na mfuko huu.
iii) Elimu ya lishe bora imekuwa ikitolewa kwa walengwa wanapohudhuria kliniki na wakati wa zoezi la malipo kwa walengwa hii itasaidia kupunguza hali ya udumavu kwa watoto.
iv) Walengwa wameweza kuanzisha miradi midogo midogo kama vile ufugaji wa kuku, mbuzi wa maziwa, kondoo, sungura, bata, nguruwe na uuzaji wa maziwa ili kujingezea kipato.
v) Pia baadhi ya walengwa wameweza kuboresha makazi yao.
vi) Uanzishaji wa kikundi cha ufugaji wa kuku katika kata ya Ruaha na kikundi cha kuweka na kukopa kata ya Kitanzini ambapo walengwa wameanza kukopeshana.
vi) Vile vile walengwa wamepata elimu ya ujasiriamali kupitia maafisa ugani waliopo katika kata.
3.1 CHANGAMOTO
Nawasilisha
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa