“Nimeamua kuachana na mchakato wa kupinga kutolewa kuwa Meya wa Manispaa ya Iringa ili vikao vya madiwani na shughuli za maendeleo za Manispaa ziendelee na wananchi waendelee kupata huduma kama kawaida”
Kauli hiyo imetolewa na aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa Ndugu. Alex Kimbe alipo pata fursa ya kuwaaga watumishi wa Manispaa ya Iringa katika ukumbi wa Manispaa.
Aidha amewashukuru sana watumishi wote kwa kufanya kazi naye bega kwa bega kwa kipindi chote alichokuwa Meya pia amewahasa wazidi kufanya kazi kwa bidii ili wafikie malengo yao hata yeye alipata sifa nzuri kupitia watumishi kwa utendaji kazi wao mzuri na ataendelea kutoa ushauri kama Diwani wa kata ya Isakalilo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa