• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

ALUTE: "HAKIKISHENI MIRADI INAKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA UBORA"

Posted on: December 21st, 2024

Katika Juhudi za Kuhakikisha Miradi ya Serikali inakamilika kwa wakati na ubora unaotakiwa, Kamati ya Ufuatiliaji wa Miradi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa imefanya ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya afya na elimu iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa lengo la kuona hatua iliyofikia na kujua changamoto zinazoathiri maendeleo.

Ziara Hiyo imefanya Ukaguzi wa Miradi ya Ujenzi wa Kituo cha Afya Kitwiru na Miundombinu katika Shule ya Sekondari Kwavava (Kata ya Kitwiru), Mabweni 2 kwa wenye mahitaji maalumu - Shule ya Msingi Ipogolo (Kata ya Ruaha), Ujenzi wa Kichomea taka, Stoo ya Dawa na Jengo la Upasuaji Hospitali ya Frelimo, Bwalo la Chakula Shule ya Sekondari ya  Kwakilosa (Kata ya Kwakilosa), Jengo la Kitega Uchumi (Kitanzini Community Welfare) na Choo katika Shule ya Sekondari Miyomboni (Kata ya Kitanzini).

Kiongozi wa Timu hiyo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Mipango na Uratibu, Mchumi John Alute amesema kuwa lengo la Ziara hiyo ni kuangalia hali ya Maendeleo ya Ujenzi wa Miradi hiyo na kuangalia changamoto zilizopo ili zitatuliwe kwa wakati na hatimaye Miradi hiyo kukamilika kwa ubora na muda uliopangwa ili ikawahudumie wananchi.

Hata hiyo muendelezo wa ziara hiyo umeongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Elias Mvula pamoja na Wataalamu mbalimbali wamefanya Ukaguzi wa Miradi ya Ujenzi wa vyoo katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Shule ya Msingi Mkimbizi, Shule ya Msingi Mgongo, Shule ya Msingi Kipululu, Shule ya Msingi Gangilonga na Zahanati ya Nduli.

Vilevile, Timu hiyo imekagua Ujenzi wa Shule mpya ya  Sekondari Makorongoni  katika Kata ya Nduli (Chini ya Mradi wa SEQUIP) ambapo inaendelea na Ujenzi wa Jengo la Utawala, Madarasa 4, Vyoo, Maktaba,  Maabara ya Fizikia, Bailojia na Kemia. Pia, wamefanya Ukaguzi kwa umaliziaji wa vyumba vya Madarasa, Ofisi na Nyumba ya Walimu S/Msingi Kigonzile na Ujenzi wa Bwalo la Chakula Shule ya Msingi Mapinduzi. ambapo, Miradi yote ipo katika hatua nzuri.

Aidha, Mvula Amewataka Wasimamizi wa Miradi hiyo kuhakikisha wanaikamilisha kabla ya Disemba 31, 2024 kama agizo la Mkuu wa Mkoa linavyosema, pia amewashauri wamtumie Mhandisi wa Halmashauri katika kufanya tathmini za gharama zinazotakiwa kwenye Miradi ili kuhakikisha thamani ya fedha za Mradi inaendana na ubora wa miradi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUONGEZWA MUDA WA KUCHUKUA FOMU YA UJENZI WA JENGO LA BIASHARA TEMBO BAR February 15, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA, 2023/2024 July 13, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI July 17, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI July 23, 2024
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • PPP CENTRE YATOA MAFUNZO KWA WATAALAMU IRINGA MC

    April 04, 2025
  • ALUTE: "HAKIKISHENI MIRADI INAKAMILIKA KWA WAKATI NA KWA UBORA"

    December 21, 2024
  • UCHAGUZI HURU NA WA HAKI UNAHITAJI USHIRIKISHAJI - RC SERUKAMBA

    October 10, 2024
  • MSIGALA AWAONYA MAAFISA MAENDELEO KUJIHUSISHA NA MIKOPO HEWA

    October 05, 2024
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA,2023/2024
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa