“Tumeongeza muda wa wafanyabiashara kufanya kazi katika Masoko yote ndani ya Manispaa kuanzia saa Kumi na mbili Asubuhi mpaka saa Tatu usiku isipokuwa kwa wale wafanyabiashara wa Vizimba ilikuongeza Uchumi wa Manispaa ya Iringa”
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Joseph Ryata katika kikao cha Baraza la Madiwani la kupitia taarifa za kipindi cha robo ya tatu katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa
Aidha Agenda mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu Januari – Machi 2020 na taarifa ya kudhibiti UKIMWI kwa kipindi cha robo ya tatu Januari – Machi 2020.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa