Baraza la Madiwani la kupokea taarifa za kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa limepitia taarifa za mafanikio ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kata zote kumi na nane (18) za manispaa ya Iringa kwa kipindi cha robo ya tatu (Januari-Machi ,2017) tarehe 10/ 05/2018 katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa .
Baraza hilo limeongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mh. Alex Kimbe kwa kushirikiana na kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Iringa , pamoja na watendaji wa kata zote na wataalamu kutoka manispaa .
Katika kikao hicho wamewaagiza wataalamu kuleta katika kikao kinachofuata maeneo yote ya manispaa yaliyopimwa na ambayo hayajapimwa ili kuweza kuchukua hatua kwa maeneo ambayo hayajapimwa kuchukua hatua kabla maeneo hayo ya taasisi hayajavamiwa.
Mh. Kimbe amewapongeza wote walioleta taarifa katika baraza hilo na kuahidi kufanyia kazi baadhi ya changamoto zilizojitokeza.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa