Mkurugenziwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Kastori Msigala ametoa siku 7 kwawafanyabiashara wote ambao hawajalipa kodi mbalimbali za Halmashauri kufanyahivyo mara moja na baada ya muda huo kupita hatua za kisheria zitachukuliwadhidi yao.
Msigala amesema hayo akiwa kwenye ziara inayojulikana kwa jina la MTAA KWA MTAA NAMSIGALA kwa kutembelea biashara zote zilizopo katika Kata ya Gangilonga kwalengo la kukagua leseni za biashara, ushuru wa huduma na ushuru wa taka.
“Manispaaya Iringa inatakiwa kukusanya jumla ya shilingi Bilioni 6 na Milioni 700 kwamwaka wa fedha 2023/2024, ili iweze kufikia malengo hayo nimeona ni lazima kutambuakila biashara iliyopo Manispaa, hivyo hivi sasa tumefikia Kata ya Gangilongaili kukagua leseni za biashara, malipo ya mabango yote, malipo ya kodi naushuru wa huduma na taka kwa lengo la kuhakikisha tunafikia asilimia 100 katikaukusanyaji wa mapato” Amesema Msigala
Ameongezakwa kusema muitikio wa ulipaji ni mkubwa na kusisitiza wale ambao hawajalipa,kulipa mara moja kwani tayari wote wameshapewa taarifa (Demand note).
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa