Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Mheshimiwa Ibrahim Ngwada amejivunia kuongezeka kwa zahanati na vituo vya afya ndani ya Halmashauri.
Mstahiki Meya, ameyasema hayo kwenye mkutano wa Madiwani uliofanyika katika Kata ya Mlandege inayoongozwa na Diwani Mhe. Jackson Abraham Chaula.
“Kwa sasa Halmashauri tuna vituo vya afya vinne (4), na zahanati tatu (3), pia huduma za X-ray pamoja na CT-Scan kwa sasa zinapatikana hapa hapa Iringa katika hospitali yetu ya Mkoa. Vile vile, tuna kiwanda cha vifaa bandia vya binadamu, hivyo hatuna haja ya kwenda Muhimbili, au Benjamini kwa huduma hizi”. Amesema Ngwada
Vituo vya Afya na Zahanati ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Kituo cha Afya Ngome Kata ya Kihesa
Kituo cha Afya Ipogolo Kata ya Ruaha
Kituo cha Afya Mkimbizi Kata ya Mkimbizi
Kituo cha Afya Itamba Kata ya Mkwawa
Zahanati ya Mtalagala ndani Kata Ya Nduli
Zahanati ya Mkoga Kata ya Isakalilo
Zahanati ya Ugele Kata ya Mkimbizi
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa