Kamanda Mkuu wa Jeshi la Police Mkoa wa Iringa Bw. Juma Bwire amewataka Wananchi Manispaa ya Iringa walioripoti wizi wa mali mbalimbali kufika kituo cha police ili kuangalia mali zao zilizoibiwa.
Kamanda Bwire ametoa wito huo Ofisini kwakwe baada ya kukamata mali hizo katika maeneo tofauti tofauti ya mkoa wa iringa na kuwataka wananchi wawe wanatoa taarifa kwenye vyombo vya sheria pindi wanapopatwa na matatizo ya wizi katika makazi yao na sio kukaa kimya.
Kamanda Bwire amewatoa hofu wananchi wa mkoa wa iringa juu ya hali ya usalama ipo vizuri na wanaendelea na kazi ya kuhakikisha hakutokei hali yoyote ya uvunjifu wa amani.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa