Kamishna wa viapo Mh.Nicholaus Mwakasungura amewataka mawakala wa vyama vya siasa kutii sheria na kanuni za uchaguzi ikiwa ni kanuni ya 16(1)(a) ya uchaguzi wa Rais na Wabunge na 12(1) (a) na kanuni ya 42(4) ya uchaguzi wa Madiwani ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru na wa haki.
Mh. Nicholaus ametoa wito huo katika tukio fupi la kuwaapisha Mawakala wa vyama vya siasa watakao simamia uchaguzi mdogo wa madiwani kata ya Mwangata
Aidha Mawakala wa vyama vilivyo shiriki ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika ukumbi wa Olofea uliopo katika Kata ya Kitanzini Manispaa ya Iringa.
Kamishna wa viapao amewataka mawakala wote walioapishwa kufanya kazi kwa ushirikianao bila kuangalia itikadi za vyama katika Uchaguzi mdogo wa Madiwani Kata ya Mwangata unaotarajia kufanyika siku ya jumapili tarehe 12/08/2018.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa