Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi ametoa muda wa siku saba (7) kwa kampuni ya ujenzi ya Home Africa Investment Corporation kukamilisha na kukabidhi kwa Manispaa ya Iringa mradi wa Soko la kisasa la Mlandege linalojengwa katika kata ya Mlandege, Manispaa ya Iringa
Mheshimiwa Hapi ametoa agizo hilo katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi huo ambapo aliitaka kampuni ya home Africa kuzingatia muda wa mkataba na kukamilisha Soko hilo ili kufungua milango ya Kiuchumi na biashara kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa
Aidha ziara hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu , Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa