Naibu Waziri wa Tamisemis Mh, Josephat Sinkamba Kandege amewapongeza wauguzi wa Hospital ya Frelimo kwa huduma nzuri zinazotolewa kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kwa ajili ya kupata matibabu.
Haya ameyasema katika Ziara yake ya kutembelea miaradi miwili ya maendeleo ya Manispaa ya Iringa ambayo ni Machinjio ya kisasa iliyopo Ngelewala pamoja na Hospitali ya Frelimo.
Aidha Mheshimiwa Josephat Sinkamba Kandege amewataka wataalamu wa Manispaa ya Iringa pamoja na wauguzi wa Hospitali ya Frelimo kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuendelea kutoa huduma kwa wagonjwa ndani ya Manispaa na nje watakaofika hospitalini hapo.
Mwisho amewashukuru wote walioshiriki katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo Manispaa ya Irirnga.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa