Mstahiki Meya wa Halmshauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amewahutubia wananchi wa Kata ya Mkimbizi na kuwataka watendaji na Wenyeviti wa mitaa kuwahudumia wananchi pasipo kilipishwa fedha yoyote ile.
“Ni marufuku kwa Mwenyekiti au Mtendaji yeyote kumtoza mwananchi hela yoyote anapokuja kupata huduma kwa kisingizio cha fedha ya Mihuri, Karatasi au Wino kwani vitu vyote hivyo vimetolewa na serikali nchi nzima ili wananchi wapate huduma kiurahisi”. Amesema Ngwada
Aidha Diwani wa Kata ya Mkimbizi Mhe. Eliudi Peter Mvella amewaasa wakazi wa Kata hiyo wasiongopewe na watu wengine kwa kigezo cha wao hawajaleta maendeleo yoyote nchini, kwani kila kitu kipo wazi na miradi mikubwa inatekelezwa na inaonekana hivyo wasikubali kuyumbishwa kwa namna ya yoyote ile.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa