Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga ametembelea na kukagua huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Frelimo jana Tarehe 28.05.2021
Ziara yake hiyo iliwahusisha viongozi wa Serikali ambao ni ndugu Happiness Seneda Katibu Tawala Mkoa pamoja na Ndugu Hamid Njovu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Iringa wengineo
Akizungumza na baadhi ya wagonjwa waliohudhuria kupata matibabu Hospitalini hapo (wakina mama waliofika kliniki) amesema, wakina mama wanatakiwa kuwalinda watoto wao na kuhakikisha wanapata malezi bora ambayo yatakuwa faida kwa familia zao na Nchi kwa ujumla hapo badae
Christina James ambaye ni mmoja wa waliofika kuhudumiwa Hospitalini hapo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwatembelea na amemwomba aendelee kufanya ziara kama hizo ili kujua changamoto zilizopo kituoni hapo na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka kwa manufaa ya Wananchi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa