• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Miji
      • Elimu Sekondari
      • Elimu Msingi
      • Afya
      • Maji
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Environment and Cleaning
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Kazi
    • Vitengo
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji nyuki
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Ufugaji
    • Kilimo
  • Huduma zetu
    • Huduma ya elimu
    • Huduma ya Afya
    • Huduma ya Maji
    • Huduma ya kilimo
    • Huduma ya Uvuvi
    • Huduma ya Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Vikao
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati wa Halmashauri
    • Ripoti
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya picha
    • Video za shughuli za ofisi au Kitaifa
    • Hotuba

UBAKAJI,ULAWITI SASA BASI-MSTAHIKI MEYA MANISPAAA IRINGA

Posted on: July 6th, 2022

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.Ibrahim Ngwada amefanya kikao na viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini leo siku ya ijuma tarehe 6/7/2022 katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Iringa, lengo la  kikao hicho ikiwa ni kujadili mustakabali wa masuala ya ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake.

Akifungua kikao hicho Mhe.  Ngwada amefurahishwa na muitikio mkubwa wa viongozi hao na kusema kuwa lengo la kikao hicho ni kujadili jinsi ya kutatua na kukabiliana na na changamoto kubwa ya mmomonyoko wa maadili hususani ulawiti na ubakaji uliokithiri dhidi ya watoto na wanawake katika Manispaa ya Iringa.

Aidha Mhe.Ngwada amesema kumekuwa na ongezeko kubwa sana la kesi za ulawiti ambazo zimekuwa zikiripotiwa polisi Dawati la Jinsia jambo ambalo limepelekea kuwaomba viongozi hao wa dini kulichukua jambo hili ili waweze kuona namna bora ya kupambana na  hali hii iliyopo kwa sasa ikiwa ni kwa kutoa elimu zaidi ya kiroho kwa kuwaasa waumini kuacha kabisa matendo hayo maovu ambayo hayampendezi Mwenyezi Mungu pamoja na wanadamu.

Afisa ustawi wa jamii Bi. Tinieli Mbanga ameeleza kuwa walianza kutekeleza afua za ulinzi kwa watoto mwaka wa fedha 2017 – 2018 na ametaja kuwa jumla ya matukio 4651 yameripotiwa ambayo yalihusisha vitendo vya ubakaji, ulawiti kwa watoto, wanawake na vijana kwa ujumla.

Mbaga amesema kuwa njia wanazo zitumia kukabiliana na suala hilo ni kutoa elimu kwa jamii, kuanzisha kamati ya ulinzi na usalama kwa watoto, mpango wa marekebisho wa tabia, makongamano na mikutano ya hadhara

Bw.Justus Basike Mkaguzi Msaidizi wa polisi amesema  kuwa wamekuwa wakishughulikia kisheria vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji na ulawiti, na kuwa changamoto wanazo kumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ni ucheleweshwaji wa taarifa na wanafanilia kushindwa kufika mahakamani kutoa ushahidi na kumaliza kesi majumbani.

Aidha ameeleza mbinu wanazo zitumia kukuabiliana na ukatili ikiwemo kutoa elimu ,kushirikiana na ofisi ya ustawi wa jamii ya Manispaa na kufanya doria kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo vilabu vya pombe.

Katika kikao hicho viongozi hao wa dini  kwa pamoja wameshukuru uongozi wa Manispaa kwa kuona umuhimu wao na kuwaita kujadiliana kwao ni jambo la faraja, na wameliomba Jeshi la polisi kufatilia kwa karibu vibanda umiza ambavyo vimekuwa ni kichocheo kikubwa cha  matukio hayo ya ukatili na kuweka sheria ambazo zitaweza kuwalinda watoto dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Mstahiki Meya Mhe.Ngwada amewashukuru viongozi Kwa kuitikia wito huo huku wakiunda kamati ya kupambana na ukatili na ulawiti na  kuweka maazimio ishirini na mbili( 22) ambayo yatasaidia kupunguza na kutokomeza kabisa vitendo vya ukatili katika Manispaa  hii.


Matangazo

  • IMC. TANGAZO LA KUITWA KWENYE KAZI ZA MUDA YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022 July 27, 2022
  • TANGAZO LA NAFASI ZA VYUMBA VYA BIASHARA KATIKA STENDI YA IGUMBILO March 10, 2022
  • TANGAZO LA KAZI MANISPAA YA IRINGA 30.05.2022 May 30, 2022
  • IMC. MIRADI YA UVIKO HADI TAREHE. 3 JAN 2022 PDF January 04, 2022
  • Soma zote

Habari za Hivi punde

  • MANISPAA YA IRINGA ILIVYOFANIKIWA KWA MWAKA WA FEDHA 2021/2022

    August 17, 2022
  • SAMIA KUTOA M.700 KUJENGA SOKO LA MACHINGA MANISPAA YA IRINGA

    August 12, 2022
  • MANISPAA YA IRINGA YATIA FOLA MAPOKEZI YA RAIS SAMIA

    August 11, 2022
  • VIJANA UMISETA MKOA WA IRINGA WAJIPANGA KURUDI NA USHIINDI 2022

    August 04, 2022
  • Soma zote

Video

MEYA WA MANISPAA KUZIPIGANIA TIMU ZA MKOA KUPANDA DARAJA
More Videos

Viunganisho vya Haraka

  • National Examination Council of Tanzania
  • Watumishi Portal
  • Sheria ndogo za Manispaa
  • Vivutio vya Utalii na Taarifda zake
  • Taarifa kwa vyombo vya Habari

Tovuti Zinazofanana

  • Goverment Website
  • TAMISEMI
  • Iringa Region Website
  • IMtv Fahari ya Iringa

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

Location Map

Wasiliana nasi

    Iringa Municipal Council

    Sanduku la Posta: 162

    Telephone: +255-2702647

    Mobile: 255-2702647

    Email: md@iringamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya usiri
    • Ukanusho
    • MMM
    • Ramani ya eneo
    • Huduma zetu

hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa