Kaimu Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti UKIMWI Mh Sarah Mwajeka Amewataka wataalamu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Iringa kutoa Elimu kwa vikundi mbalimbali vya wajasiliamali vilivyopo Manispaa ya Iringa ili kukuza mitaji na faida
Mh Mwajeka ametoa kauli hiyo katika ziara ya kamati ya kudhibiti UKIMWI iliyofanyika mapema leo ambapo ilitembelea miradi mbalimbali ikiwemo kikundi cha Matumaini kilichopo kata ya Kihesa pamoja na kituo cha upimaji wa wingi wa Virus vya UKIMWI kilichopo Hospitali ya Mkoa wa Iringa.
Mbali na hayo amewataka wataalamu wa Kilimo na ufugaji kutoa elimu juu ya matumizi ya viwatilifu kwa wakulima na wafugaji ili kuchochea kilimo chenye tiba
Ziara hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Manispaa pamoja na timu ya Menejimenti Manispaa ya Iringa
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa