Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mh. Alex Kimbe amewataka wataalamu wa Afya Manispaa ya Iringa kuongeza juhudi za kutoa elimu kwa wananchi kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Mh.Kimbe ametoa agizo hilo katika kikao cha wazi cha Baraza la madiwani la kupitia taarifa ya robo ya tatu kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa, ambapo agenda mbalimbali zimejadiliwa ikiwemo kupitia kamati za kudumu, taarifa ya kudhibiti UKIMWI, taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Aidha amewapongeza wananchi wote waliojikeza kushiriki katika baraza hilo la wazi la kupokea taarifa kutoka katika Kata zote kumi na nane na kuwataka kuwa na moyo wa kufuatilia vikao mbalimbali ili kujua muelekeo wa Halmashauri.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa