Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amewaagiza Watendaji wa Kata kutoka Manispaa ya Iringa kuendelea kuhamasisha jamii kutumia unga wenye virutubishi na ikiwezekana kupita nyumba kwa nyumba ili kuhamasisha lishe bora ili kuondoa utapiamlo kwa watoto katika Manispaa hiyo.
Mhe. Richard Kasesela ameyasema hayo wakati wa mkutano wa tathimini ya utekelezaji wa viashiria vya mkataba wa lishe ngazi ya Kata na Mitaa ya robo ya kwanza 2020/2021 kilichofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria,
Ameendelea kwa kusema ni aibu kwa Mkoa wa Iringa kuwa na asilimia 47 ya Utapiamlo kwani kuna kila aina ya vyakula vya lishe.
Kwa upande wake Afisa lishe kutoka Manispaa ya Iringa Bi. Anzaeli Msingwa amewaasa wanaume kujiwekea mazoea ya kutenga muda wa kuongea na mtoto wake akiwa bado tumboni ili kujenga afya bora ya mtoto.
“Akina baba mhakikishe mnawajengea uchangamfu Watoto tangu wakiwa tumboni kwa mama ili kuwafanya wajue mazingira tofauti ya nje”.
Kwa upande wao baadhi ya Watendaji wa Kata wamesema changamoto inayofanya Kata zao kuendelea kuwa na watoto wenye utapiamlo ni upatikanaji wa walengwa kwani wanapotembelea hawawakuti na wanashindwa kupata takwimu sahihi.
Katika kikao hicho wamejiwekea mkakati wa kuhakikisha kwamba ifikapo 2025 Manispaa ya Iringa haitakuwa na Watoto wenye utapiamlo.
kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Lishe wakiwemo TAHEHA, PAPA YOHANE pamoja na watendaji kata Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa