Kamati ya Fedha na Uongozi pamoja na Wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaaya Iringa wamepatiwa mafunzo kuhusiana na elimu ya uwekezaji wa miradi baina ya sekta za umma na sekta binafsi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina yao nakutengeneza mazingira bora ya uwekezaji katika Halmashauri, hali itakayopelekea ongezeko la mapato na ukuaji wa uchumi.
Mafunzo hayo yametolewa Aprili, 03 2025 na Wawezeshaji kutoka Kituo cha Ubia baina ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP Centre) Dkt, Moshi Derefa na Ziada Saburi katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Iringa.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amewashukuru wawezeshaji hao kwa elimu waliyoitoa kwani itaboresha mazingira ya uwekezaji katika miradi ya Halmashauri na itaongeza mapato ya ndani na serikali kiujumla. Vilevile, ametoa agizo kwa wakuu wa Idara na Vitengo kuainisha miradi waliyonayo ili iweze kuandikiwa taarifa kwaajili utekelezaji.
Baadaya mafunzo hayo, Timu ya wawezeshaji pamoja na Wataalamu wamepata nafasi yakutembelea maeneo mbalimbali ya uwekezaji katika Manispaa ya Iringa kwa lengola kupata maelezo ya mradi, kujua mahali mradi ulipo kwa kusoma majira nukta (coordinates) ili kupata maelezo ya kutosha na hatimaye waone ni namna gani wanavyoweza kuishauri Halmashauri namna bora ya uwekezaji.
Kituo cha Ubia cha PPP Centre kinaratibu na kusimamia masuala ya ubia baina ya sekta za Umma na Binafsi nchini kwa mujibu wa sheria ya ubia baina ya sekta ya umma na sekta binafsi, sura 103 kupitia kifungu cha 4 (1) ambapo kwa sasa kinaendelea na utoaji wa elimu nchini katika mikoa 13, huku Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ikiwa ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa