Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Peter Serukamba amewataka Watendaji wa Kata na Mtaa waliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja katika kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili uwe huru na wa haki.
Ameyasema hayo, katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Oktoba 09, 2024 katika kikao kazi na maafisa mbalimbali wa Serikali hasa wanaohusika katika zoezi zima la Uchaguzi wakiwemo Maafisa uchaguzi ngazi ya Halmashauri, Tarafa na Ka, maafisa watendaji Kata na Mitaa waliopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ambao wanashiriki kusimamia zoezi la uandikishaji na upigaji
wa kura kwa wakazi wa Halmashauri hiyo.
" Kuanzia Tarehe 11-20 Oktaba, 2024 tunaanza zoezi la Uandikishaji wa wananchi kwenye orodha ya wapiga kura kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.,Sisi tunaosimamia uchaguzi huo, ni jukumu letu kuhakikisha watu wamejiandikisha, kuhakikisha watu wamefanya kampeni vizuri, kuhakikisha vyama vimepewa nafasi sawa kwenye kushiriki uchaguzi huu pamoja na kuhakikisha kuna Usalama na amani kwa muda wote mpaka kumaliza uchaguzi hapo Tarehe 27/11/2024.". Amesema Serukamba.
Serukamba amesema kuwa ili Uchaguzi uwe huru na wa haki lazima uwe shirikishi ikiwa ni pamoja na wananchi kushirikishwa kwa kuonyeshwa vituo vyao vya kujiandikisha na vya kupigia kura, vilevile vyama vya
siasa vishirikishwe katika zoezi zima la uchaguzi ili itakapofika mwishoni vyama viridhie matokeo.
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inatarajia kuwa na idadi ya watu 126,000 ambao watajiandikisha na kupiga kura.,hii ni kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2022 ambapo idadi hiyo ya watu walivuka umri wa miaka 18.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa