UTANGULIZI
Idara ya Mipango Takwimu na Ufuatiliaji ni moja kati ya idara 13 zilizopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. Idara hii ina jumla ya watumishi 6 kama wanavyoonekana hapa chini;
S/N
|
CHEO
|
1.
|
Mchumi wa Halmashauri
|
2.
|
Mchumi Mwandamizi
|
3.
|
Mchumi I
|
4.
|
Mtakwimu I
|
5.
|
Mtakwimu I
|
6.
|
Mchumi II
|
MAJUKUMU YA IDARA YA MIPANGO TAKWIMU NA UFUATILIAJI
Idara hii ina majukumu mbalimbali lakini majukumu ya msingi ni kama
yanavyooneshwa hapa chini;
MAFANIKIO YA IDARA
4.0 MATARAJIO YA IDARA
Idara hii ina mipango na matarajio makuu kama inavyoonekana hapa chini
Wananchi wanawezeshwa kuibua miradi itayoweza kutekelezeka na yenye manufaa kwao na Halmashauri kwa ujumla
Kuhakikisha Halmashari inakuwa na mipango na bajeti na utekelezaji wake unafanyika kulingana na vipaumbele na upatikanaji wa rasilimali
Kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kushirikiana na Idara zinazotekeleza mradi husika
Halmashauri inakuwa na takwimu sahihi, zilizochambuliwa, kutunzwa na kutolewa kwa wateja mara zinapotakiwa.
Kuandaa maandiko na kuyauza kwa wadau kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Kuwa na Investment Profile inayoenda na wakati sambamba na Investment menu ya Halmashauri ambapo kila mtu mwenye nia ya kuwekeza atapata taarifa zote na hivyo kupelekea urahisi wa kuwavutia wawekezaji.
5.0 HITIMISHO
Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji ni kiungo cha Idara zote katika utekelezaji wa shughuli za kawaida na Miradi ya Maendeleo ya halmashauri, hivyo hufanya kazi kwa ukaribu na Idara zote zilizopo Halmashauri sambamba na wadau wote wanaohusika na idara hizo. Kwa nafasi hii, Ofisi inawakaribisha wadau wote ili kutoa mawazo ya kuboresha huduma zinazotolewa kwa faida ya Halmashauri yetu, mkoa na Taifa kwa ujumla.
Naomba kuwasilisha,
IDARA YA MIPANGO TAKWIMU NA UFUATIKLIAJI
MANISPAA YA IRINGA
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa