Katika ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) mkoa wa Iringa imefanya ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na Manispaa ya Iringa ambayo ni mradi wa Ujenzi wa stendi ya mabasi Igumbilo na mradi wa soko la kisasa la Mlandege.
Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa ALAT mkoa wa Iringa ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa ALAT Taifa ndugu Stephen Mhapa amesema lengo la kuzungukia miradi ni kujionea jinsi ambavyo serikali za mitaa zinatekeleza miradi yake na kutoa ushauri na baadae kama kutatokea changamoto basi taarifa zitawasilishwa ALAT Taifa kwa utekelezaji zaidi.
Amesema lazima serikali za mitaa ijivunie miradi inayosimamiwa na kutekelezwa na serikali za mitaa kwani ni miradi mizuri na ina manufaa kwa wananchi wa Tanzania.
Naye katibu wa ALAT mkoa wa Iringa ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo Ndugu Aloyce Kwezi amesema, ni muhimu sana wakati wa vikao vya ALAT Taifa vinafanyika masuala yote ambayo ni changamoto kwa Halmashauri yawasilishwe ili kuweza kupata ufumbuzi kwani kikao cha ALAT Taifa kinatarajiwa kufanyika tarehe 24/9/2018, hivyo ni fursa muhimu kwa wajumbe wa ALAT Taifa kuwasilisha changamoto.
Ziara hiyo imehudhuriwa na wajumbe wa ALAT kutoka katika wilaya zote za mkoa wa Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa