"Nipende kumpongeza Mkurugenzi na wataalamu wake kwa kazi nzuri ambayo wameifanya katika shughuli za kimaendeleo katika Manispaa yetu ya Iringa"
Hayo yamezungumzwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada tarehe 12.02.2021 katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la kupitisha mapendekezo ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2021/2022 uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri
"Mwaka huu lazima eneo la Tembo Bar lijengwe ili kujiongezea mapato yetu katika Halmashauri kwa kupitia sisi wenyewe au wawekezaji" Mh. Ngwada alisema hayo kama moja ya lengo lake kubwa ambalo anahitaji litime kwa kipindi hiki cha mwaka huu wa 2021
Hata hivyo katika maelezo yake amesema vipaumbele vyake vingine ambavyo anatamani vikamilike ni pamoja kuendeleankutoa mikopo kwa walemavu, ujenzi wa soko la nyama la Kitwiru pamoja na Ujenzi wa jengo la jumba la maendeleo (Community Centre)
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu amepokea changamoto mbalimbali za Madiwani hao na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo
Naye Mkuu wa Idara ya Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Ndugu Herbert Bilia ameipongeza na kuishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa namna wanavyojitoa katika masuala ya kimaendeleo nchini hasa katika Halmashauri hii kwa kupatiwa fedha mbalimbali kwa shughuli za kimaendeleo
Akifunga kikao hicho Mstahiki Meya Mh. Ngwada, amewataka waheshimiwa Madiwani wenzake, watendaji wa Kata pamoja na wataalamu wa Manispaa kuzidi kufanya kazi kwa juhudi katika kuiletea Maendeleo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Pia amemshauri Mkurugenzi kuendelea kukamilisha miradi yote ya maendeleo iliyoanzishwa ndipo kuanza kutekeleza miradi mipya ili kuepusha hasara inayoweza kujitokeza kwa miradi hiyo kuachwa na kuchakaa
Nae Juli Sawami ambaye ni Diwani wa kata Kihesa amempongeza Mkurugenzi kwa hatua aliyofikia katika umaliziaji wa ujenzi wa majengo ya madarasa na amempongeza Mstahiki Meya kwa jitihada za kutafuta madawati 500 kwa wadau mbalimbali katika kupunguza changamoto ya madawati katika sekta ya elimu ndani ya Manispaa
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa