Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa likiongozwa na Mstahiki Meya Mhe. Ibrahim Ngwada limejadili mpango wa Bajeti ya Halmashauri unaogharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 46,010,462,000/= kwa mwaka wa fedha 2024/2025
Akiwasilisha taarifa ya bajeti ya Halmashauri katika kikao hicho, Mchumi wa Manispaa Ndg, Abel Ndeabura amesema kuwa fedha hizo zinatokana na Ruzuku kutoka serikali kuu na mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo, mishahara ya watumishi na matumizi ya ofisi.
Miongoni mwa vipaumbele ambavyo vimetajwa kwenye bajeti ni pamoja na kuboresha miundombinu ya Sekta ya Elimu hasa Kwa kutengeneza madawati,viti na meza za walimu, Afya, Umeme na Maji, kuweka Mazingira ya Mji safi kwa kuzoa taka ngumu zinazozalishwa katika Masoko, kujenga na kuboresha barabara za Mitaa(TARURA), kuanzisha Miradi na kuboresha miundombinu sekta ya biashara na Masoko kama vile kuanzisha Machinjio ya Kuku, kupitisha azimio la uwekezaji Stendi ya zamani Tembo Bar, pamoja na Utoaji wa mikopo asilimia 10 kwa makundi maalumu ya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu
Aidha, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhe.Ngwada amemuagiza Mkurugenzi kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa maazimio yote yaliyotolewa kwenye kikao hicho ili baheti hiyo iweze kukidhi mahitaji ya Halmashauri.
.
Aidha Ngwada amesisitiza kuwa katika Sekta ya Elimu bajeti ya Madawati iongezeke ili kumaliza tatizo la upungufu wa madawati Mashuleni.
"Kwenye kikao cha kamati ya Afya, Uchumi na Elimu tulikubaliana bajeti ya Madawati iongezeke kutoka sh. milioni 25 hadi milioni 150 na kuendelea ili kuondoa tatizo la m
Madawati kwenye Shule zetu zote za Msingi na Sekondari zilizopo hapa Mjini Iringa". Amesema Ngwada.
Dr.Godfrey Mbangali ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na atayafanyia kazi kwa ajili ya maboresho ya mpango wa bajeti hiyo kwa maendeleo ya Halmashauri na wananchi kwa ujumla.
Kikao hicho cha Baraza Maalum la kujadili mpango wa bajeti kwa mwaka wa Fedha 2024/2025 kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Taasisi chama na Serikali, wakuu wa Idara na vitengo, wananchi na madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa umefanyika Januari 24 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Manispaa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa