Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Ally Hapi ameupongeza Uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na wadau wa Manispaa kwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 ikiwa ni Miaka minne mfululizo kutokana na taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
“Hii inaonyesha Baraza la Madiwani, Mkurugenzi Pamoja na wataalamu wote wa Manispaa mnafanya kazi kwa kujituma na kufuata vigezo na malengo mliyojiwekea.”
Amesema Miradi ya maendeleo ambayo imeanza imaliziwe na huduma kwa wananchi ziendelee kutolewa kwa viwango ili wananchi wazidi kuipenda serikali na kuchangia mapato kwa huduma bora wanazozipata.
Mkuu wa Mkoa Mheshimiwa Ally Hapi amesema kipimo cha watumishi ni jinsi ambavyo tunaweza kusimamia utekelezaji wa Miradi yetu ya Maendeleo, hivyo amewaomba watumishi kufanya kazi kwa badii kusimamia miradi ya maendeleo na kuibua vianzia vipya vya mapato.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa