Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa limefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2022/2023 kwa lengo la kuona maendeleo ya miradi hiyo kuona na kutatua changamoto zinazojitokeza wakati wa ujenzi.
Ziara hiyo imefanyika leo tarehe 10 Mei ikiongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe.Ibrahim Ngwada ambaye alisisitiza ukamIlishaji wa miradi hiyo kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika nayo.
'Naagiza kuanzia tarehe 15/5/2023 mama na baba lishe waanze kutumia eneo la Mgahawa kutoa huduma ya chakula kwa abiria alisema Ngwada.'
Ngwada ametoa maelekezo hayo kwa Menejimenti ya Halmashauri wakati wa ziara walipokuwa wakikagua Jengo la Utawala stendi ya Igumbilo.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa ni pamoja na Mendeleo ya stendi ya Igumbilo,ujenzi wa Shule mpya ya Kitwiru, Miundombinu ya vyoo shule ya msingi Igumbilo, Miundombinu ya Machinga Katika eneo la Mlandege,Miundombinu ya Hospitali ya Frelimo na miundombinu ya shule ya msingi Gangilonga na Mapinduzi.
Charles Mwaitege ni Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na waheshimiwa Madiwani na kuahidi kuyafanyia kazi.
Ziara hiyo ya siku moja iliwashirikisha Madiwani wa Manispaa pamoja na wakuu wa Sehemu na vitengo.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa