Baraza la wazi la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa limepitia taarifa za mafanikio ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo kwa kamati zote za kudumu za Manispaa ya Iringa kwa kipindi cha robo ya pili (oktoba-desemba,2017) tarehe 6/ 02/2018 katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa .
Baraza hilo limeongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mh. Alex Kimbe kwa kushirikiana na kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Iringa , pamoja na Mkuu wa wilaya na katibu Tawala wilaya ya Iringa ambapo wamepokea taarifa mbalimbali kutoka kwenye Kamati za kudumu za Manispaa ya Iringa. Na kuzipongeza kamati kwa jitiada walizozifikia huku wakiwataka Madiwani pamoja na Watendaji wa Kata kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi.
Mbali na hayo Baraza limewaapisha Madiwani wanne kupitia jaji wa serikali kikatiba ambapo madiwani wawili ni kutoka viti maalumu na wengine wakuchaguliwa na wananchi kutoka kata ya kitwiru pamoja na kata ya kihesa kisha kuruhusiwa kuanza kazi rasmi za kiutendaji kwenye kata zao na kushiriki kikamilifu vikao vya mabaraza.
Mwisho Mkuu wa Wilaya Mh. Richard Kasesela alipata nafasi ya kuhitimisha na kutoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Meya wa Manispaa pamoja na wakuu wa Idara kwa kufanya kazi kwa ushirikiano bila kufuata itikadi za chama kwani maendeleo hayana chama.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa