Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa limepitia taarifa za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo katika kata zote kumi na nane (18) kwa kamati zote za kudumu za Manispaa kwa kipindi cha robo ya pili (oktoba-desemba, 2017) katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa.
Baraza hilo limeongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe kwa kupokea taarifa mbalimbali kutoka katika kamati za kudumu za Manispaa na kuwataka Madiwani pamoja na watendaji wa kata kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi .
Aidha Mh Kimbe amewaomba Madiwani wenye matatizo ya miundo mbinu kwenye Kata zao hususani Barabara waelekeze Barua za maombi ya ukarabati kwa meneja wa TARURA na sio kwa Mkurugenzi kama wanavyofanya sasa kwa lengo la kupata ufumbuzi wa haraka zaidi.
Mwisho amefunga kikao hicho kwa kuwapongeza Madiwani wote waliotoa taarifa zao za Kata kwa kufanya kazi vizuri na kushirikiana na watendaji wa kata pamoja na watendaji wa Mitaa kwa ujumla huku akiahidi kutatua baadhi ya changamoto wanazokutanao nazo katika utendaji wao wa kazi
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa