Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amwaipongeza wafanyakazi wa benki ya CRDB kwa huduma nzuri wanazozitoa kwa wananchi hususani kwa waheshimiwa Madiwani wafikapo katika ofisini zao kupata huduma mbalimbali za kibenki
Hayo ameyasema leo Jumatano Septemba 20 mwaka 2022 katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa, mbele ya viongozi wa Benki ya CRDB kanda ya kati waliotoka Mkoani Dodoma walipotembelea Ofisi za Halmashauri hii
"nimefurahishwa na ujio wenu na hakika niwapongeze kwa huduma zenu nzuri na tuna ahidi kuendelea kushirikiana nanyi kwa kila hatua hususani katika kuiletea maendeleo Manispaa yetu" Mhe. Ibrahim Ngwada alisema
kwa upande wake kiongozi wa msafara huo wa wageni Meneja wa CRDB kanda ya Kati Ndg. Chabu Mishwaro amesema amefurahishwa na mapokezi ya Ofisi ya Mkurugenzi na Mstahiki Meya na wamejifunza mengi na hivyo watahakikisha wanaendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina yao kwa manufaa na maendeleo ya wananchi wa Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa